Tanzania imepakana na nchi
Nane (8) ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo (DRC), Zambia, Malawi na Msumbiji ambazo zina mipaka ya nchi kavu
iliyorasmi na isiyo rasmi. Katika mipaka hiyo ipo iliyo nchikavu na ile ambayo
ipo ya bandari katika maziwa kama ziwa Nyasa, ziwa Tanganyika na victoria.
Biashara
katika nchi hizo na ukanda huo wa masoko hayo biashara iliongezeka kutoka dola za
Marekani milioni 688.573 mwaka 2026 sawa na TZS 1,499.093 milioni hadi dola za
Marekani milioni 2,133.422 mwaka 2021 sawa na TZS 4,529.616 milioni na ukuaji
wake ulikuwa wa wastani wa asilimia 84.7 ambao ni ufanisi mkubwa katika
biashara ya kikanda katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa faida ya
Tanzania kwa wastani wa 2.4%.
Mwenendo wa Biashara
Biashara
baina ya Tanzania nan chi hizo, imefanyika kupitia mipaka mbalimbali
ilioyorasmi ikiwemo ni pamoja na mipaka ya
Mtambaswala (Mtwara), Kasumulu (Kyela), Tunduma
(Momba), Manyovu (Buhigwe), Mabamba (Kibondo), Kabanga na Rusumo
(Ngara), Murongo (Kyerwa), Mutukula (Misenyi), Sirari (Tarime), Namanga (Longido), Tarakea na Holili (Rombo) na Horohoro (Mkinga).
Mipaka mingine ambayo inatumika ni pamoja na Nyabibuye na Nyemuhange (Kakonko), Nkenda
(Songea), Kilambo (Mtwara), Isongole mpaka wa Tanzania na Malawi
kupitia Ileje. Aidha, ipo mipaka ambayo
inapitia bandari katika bahari na maziwa ambayo hutumika sana na
Wafanyabiashara wadogo, kwa upande wa maziwa ni Mbambabey, Manda, Tungi katika ziwa Nyasa; Kasanga, Kalema na Kibirizi
katika ziwa Tanganyika; kwa ziwa Victoria mara nyingi Wafanyabiashara wadogo
wanatumia mipaka ya Mutukula na Murongo
kwenda Uganda na pia mipaka mingine mitano ya nchi kavu kwa Wafanyabiashara
wanaokwenda Kenya.
Kutokana
na mwenendo wa biashara na nchi hizo Tanzania ina urari chanya wa wastani wa
2.4% na kwa kila soko umebainisha katika kielelezo Na. 2 na mdau muhimu katika
soko ni DRC 27.2% na Rwanda 23.8% kwa kipindi cha miaka mitano kati ya 2016
hadi 2021. Kwa kuzingatia uchambuzi huo TanTrade inaendelea kujenga uwezeo
wafanyabiashara wadogo na utafutaji wa fursa za masoko ili kuwaunganisha wazalishaji
bidhaa na wanunuzi katika masoko mbalimbali ya ndani nan je.